Kuhusu Bandarini SACCOS LTD

Historia fupi ya Chama


Bandarini SACCOS ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Msingi kinachojumuisha watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania wa ngazi zote.

Chama hiki kilianzishwa na kuandikishwa kwenye daftari la Serikali tarehe 23/8/1968 kikiwa na wanachama waanzilishi 56 kutoka Bandari ya Dar es salaam, 

Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) imegawanyika katika bandari kubwa na ndogo nazo ni Dar es salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Bukoba, Mafia, Kigoma, Kyela, Makao Makuu (HQ) na Bagamoyo. 

Dira/ Maono(Vision) Ya Bandarini SACCOS LTD


Kuwa SACCOS kiongozi kwenye utoaji wa huduma na utaalamu bora wa uendelezaji wanachama katika Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo nchini Tanzania

Dhamira (Mission) Ya Bandarini SACCOS LTD


Bandarini SACCOS itaratibu kwa ufanisi katika kutoa huduma na bidhaa bora na endelevu za kutosheleza kukidhi mahitaji ya kuwaendeleza wanachama wake kwa njia ya usawa na haki katika kuinua vipato na utendaji bora wa shughuli zao.

Usimamizi wa Fedha


Chama kimechukua tahadhari ya kuwa na akaunti za kuhifadhi fedha benki pamoja na kuajiri watendaj wenye weledi wa hali ya juu.  Hesabu za chama zinakaguliwa kila mwaka na Shirika la ukaguzi (COASCO). 

Bodi ya Bandarini SACCOS LTD


Bodi ya Bandarini SACCOS LTD inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe ambao wote huchaguliwa na wanachama. Bodi hupitia taarifa zote za kamati (watendaji, kamati ya Usimamizi, Kamati ya Mikopo, Kamati ya manunuzi n,k) angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

Watendaji wa Bandarini SACCOS LTD


Watendaji ni waratibu wa shughuli mbalimbali za chama kama utoaji wa mikopo, ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo, utunzaji wa taarifa za chama, ufungaji wa mahesabu na shughuli zinginezo zinazofanyika katika chama. Bandarini SACCOS ina watendaji nane ambao ni meneja ambae ni mtendaji mkuu wa shughuli za chama, mhasibu, maafisa mkopo wawili, afisa tehama, karani, dereva na mhudumu.

jQuery Tlačítko na začiatok by William from Wpromotions.eu
Copyright © 2019 Bandarini SACCOS LTD . All Rights Reserved 
Powered by Webnode Cookies
Create your website for free! This website was made with Webnode. Create your own for free today! Get started